September 4, 2021


 UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa tukio la sherehe za uzinduzi wa jezi ambao ulitarajiwa kufanyika leo Septemba 4 umeyeyuka.

Awali Simba waliwatangazia mashabiki wao kwamba mpango wao namba moja kwenye shughuli ya kutambulisha uzi mpya itakuwa ni Septemba 4, saa 1:00 usiku.

Jana Septemba 3, Simba kupitia kwa Kaimu Ofisa Habari, Ezekiel Kamwaga waliweza kutoa taarifa ya mshtuko kwamba uzi wa Simba upo kwenye maduka yote ya Vunja Bei.

Pia iliwekwa wazi kwamba leo tukio la uzinduzi wa jezi litaendelea kama kawaida saa 1:00 na utaratibu ungetolewa leo.

Muda mchache kabla ya shughuli kufika taarifa imetolewa kwa Simba kughairi uwepo wa tukio hilo.

Taarifa hiyo imeeleza:"Tukio la uzinduzi wa jezi rasmi za Simba kwa msimu wa 2021/22 lililopangwa kufanyika leo limeahirishwa.

"Matukio yote ya sherehe sasa yatafanyika wakati wa Wiki ya Simba inayoanza Septemba 13 hadi 19.".

7 COMMENTS:

  1. Sikuizi kuna wiki ya Simba kumbe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Uzinduzi wa Kazi gani wakati unaambiwa Hamisa Mubeto kesha maliza utamnulisho wote.
      Dadekii chezea mnyama wewe☹️

      Delete
    2. Khaji Manara kama angekuwa bado yupo simba angesema yeye ndie alieifanya Kazi ya kuwahamasisha mashabiki wa Simba kutoka kwa wingi kwenda kununua jezy, please 🤧🤣🤣

      Delete
    3. Mtandao wa African Soccer Update, umekiri kuwa Simba imeshinda vilabu vingi ulaya ambavyo huuza jezi 10000 tu kwa Msimu ikiuza 42,000 ndani ya masaa 8. Haji akapige Domo huko tu.

      Delete
  2. Hahahaha aiseee watazindua nn wakati zilishajizindua kitambo! Kolo fc mnakwama wapi?

    ReplyDelete
  3. Ndio muanguko wa kishindo wa kolo fc umeanza!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic