September 4, 2021



KOCHA Mkuu wa Biashara United, Patrick Odhiambo ameweka wazi kwamba msimu ujao lazima wafanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa kwa kuwa wana kazi ya kuipeperusha bendera ya Tanzania.

Timu hiyo inatarajiwa kuutymia Uwanja wa Mkapa baada ya ule wa Kirumba kukataliwa na Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) kwa kueleza kuwa haujakidhi vigezo.

Biashara United ilianza mipango ya maandalizi ya msimu mpya ikiwa Mwanza na kwa sasa inapiga hesabu za kuja Dar.

Kocha huyo amesema:"Kitu kikubwa ambacho tunahitaji kukifanya ni kupata matokeo chanya na kuwa na kikosi imara.

"Tunashiriki kwenye mashindano ya kimataifa hivyo ni muhimu na sisi kuwa imara, kikubwa ni maandalizi na inawezekana," .

Ni mara ya kwaza Biashara United kushiriki mashindano ya kimataifa baada ya kumaliza ligi ikiwa nafasi ya nne.

Tanzania ilipata nafasi nne za uwakilishi kwa timu za kimataifa ambapo ni mbili kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na mbili kwenye Kombe la Shirikisho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic