October 8, 2021


UNAAMBIWA soka linalipa mkwanja mrefu kwa wale ambaowanafanya vizuri katika kutimiza majukumu yao na hapa leo tunakwenda kuwatazama nyota 10 wanaokunja mshahara mrefu kwa wiki.

 Ndani ya Ligi Kuu England ambayo inatajwa kuwa pendwa kuna mastaa ambao wanakunja mshahara wa maana kwa wiki kwa msimu wa 2021/22 kwenye timu zao.

Kwa upande wa namba moja ipo mikononi mwa Cristiano Ronaldo huyu ni mshambuliaji anayetajwa kuwa mahiri zaidi na ghali yupo zake ndani ya Manchester United ambapo kwa wiki anakunja pauni 510,000 sawa na bilioni 1.6.

Kevin De Bruyne huyu ni mali ya Manchester City anatajwa kulipwa pauni 400,000 sawa na Tsh. bilioni 1.25 ni kwa wiki ujue sio kwa mwezi.

Kipa wa Manchester United David De Gea naye pia yupo kwenye orodha ambapo anatajwa kukunja pauni 375,000 sawa  na Tsh. bilioni 1.17.

Mwingine ni winga Jadon Sancho huyu ni mali ya Manchester United anatajwa kukunja pauni 350,000 sawa na Tsh bilioni 1.09.

Raphael Varane wa Manchester United huyu anatajwa kukunja pauni 340,000 sawa na Tsh. bilioni 1.06 kwa wiki bana.

Romelu Lukaku mshambuliaji wa Chelsea anatajwa kukunja pauni 325,000 Tsh bilioni 1.01 kila wiki inapomeguka.

Kiungo Jack Grealish wa Manchester City huyu anatajwa kukunja pauni 300,000 Tsh milioni 938.6.

Mwingine ni mshambuliaji Raheem Sterling huyu yupo zake ndani ya Manchester City ambao ni mabingwa waetezi wa Ligi Kuu England anatajwa kuvuta pauni 300,000 sawa na Tsh. milioni 938.6.


Mfaransa N'Golo Kante kiungo wa kazi chafu ni mali  ya Chelsea yeye anakunja pauni 290,000 Tsh milioni 907.3 na yupo kwenye orodha ya wale wanaokunja mkwanja mrefu.

Yule Paul Pogba kiungo wa Manchester United ambaye mkataba wake unakaribia kumeguka huku akiwa anawindwa na timu kibao anavuta pauni 290,000 Tsh.907.3 milioni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic