October 8, 2021


 KOCHA Mkuu wa Jwaneng Galaxy, Morena Ramoreboli, amesema wanatakiwa kufanya kazi nzito ili kuhakikisha wanaiondoa Simba katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu kwani wapinzani wao hao wana kikosi bora.

Simba katika michuano hiyo, wanaanzia ugenini kwenye hatua ya kwanza kwa kucheza dhidi ya Jwaneng ya Botswana. Mechi ya kwanza ikichezwa Oktoba 17, kisha marudiano Oktoba 22.

Morena alisema: “Ninaheshimu sana uwezo wa Simba ambao wameuonesha katika miaka ya hivi karibuni, katika michuano ya kimataifa wamefika hatua nzuri, ni timu kubwa, hivyo tunatakiwa kupambana haswa ili kutimiza malengo yetu ambayo ni kusonga mbele.

“Tunayo faida ya kuanzia nyumbani, hivyo tunatakiwa kufanya vizuri katika mchezo wetu wa mwanzo, tutapambana kuhakikisha tunasonga mbele, hakuna namna nyingine zaidi ya kwenda kupambana na Simba.”

3 COMMENTS:

  1. Mwandishi acha kuandika kwa mazoea na usitutoe njiani

    ReplyDelete
  2. Wanawapa bichwa bure!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa hiyo bichwa ulitaka upewe wewe. Utaliweza?.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic