YANGA watabaki kwenye kambi yao iliyopo Avic Town Dar baada ya uongozi kuamua kufuta ratiba ya kwenda kuweka kambi Arusha kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya Ligi Kuu Bara.
Uongozi wa Yanga umeshtukia ratiba yao ya kuweka kambi Karatu wakiona ni kama watapoteza muda kwa kuwa muda uliobaki ni mchache na itakuwa vizuri kama wakibaki Dar na kuepusha gharama zisizo na msingi.
Mkurugenzi wa Mashindano wa Yanga, Thabity
Kandoro, ameliambia Championi Ijumaa: “Timu
itabaki Dar es salaam ikiwa kwenye kambi yetu
ya Avic Town, baada ya kufikia uamuzi wa
kusitisha safari ya kwenda Arusha kuweka
kambi.
“Kubaki hapa kutaipa timu nafasi ya kupumzika
na kuwapunguzia uchovu wa safari za hapa na
pale, lakini pia hapo kuna ishu ya gharama.”
Yanga inajiandaa na mechi ya tatu ya Ligi Kuu
Bara dhidi ya KMC itakayopigwa Uwanja wa
Majimaji, Songea mkoani Ruvuma Oktoba 19 na
sasa wamekuwa wakitenga muda wa kuingia
Gym.
Leo Oktoba 10 inatarajiwa kuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya JKU SC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, saa 1:00 usiku.
Viongozi wetu wanakurupuka sana katika kutoa maamuzi. Walikuwa hawajui kuhusu sababu walizotoa?
ReplyDeleteMara nyingi ndo wako hivyo mbona
DeleteSimba kaeka kambi Arusha na sisi tuweke kambi, Simba kafika robo fainali ligi ya mabingwa na sisi msimu huu tutafika hata kama tushatolewa kha..😀
DeleteWanaweweseka sana viongozi wetu hasa kwenye masuala ya mipango
ReplyDelete