October 10, 2021


 BAADA ya mchezo wa awali timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Benin leo kuna kazi ya kufanya nchini Benin.

Watanzania wengi kwa sasa wanausubiri mchezo huo ambao unatarajiwa kuchezwa mchana huku hali ya hewa ya nchini Benin ikiwa ni ya joto.

Kutokana na hali hiyo, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania,Taifa Stars, Kim Poulsen ameweka wazi kuwa hilo kwake haoni kama ni tatizo kikubwa ambacho anahitaji ni kuona timu inashinda.

"Kwetu sisi hali hiyo haina tatizo wala sio kikwazo kwani ni hali ya hewa ambayo inafanana na kule kwetu Tanzania, uzuri ni kwamba ligi ya kule inachezwa muda huo," .

Kwa sasa tayari kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kimeshaondoka kutoka hotelin kuelekea kwenye mji wa Cotonou, Benin kwa ajili ya mchezo huo unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 10:00 kwa saa za Afrika Mashariki.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Benin, Michel Dussuyer amesema kuwa wachezaji wake wanacheza sana kwenye muda wa baridi.

"Nafikiri itakuwa changamoto kwa wachezaji wangu kwa kuwa wamezoea kucheza kwenye baridi ila ikiwa jioni na hakutakuwa na jua kali hilo halitakuwa tatizo," amesema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic