October 10, 2021


KUELEKEA tamasha la Singeli Festival kamati ya 
maandalizi imetoa idadi ya wasanii 20 wa singeli ambao watatoa burudani katika tamasha hilo litakalofanyika Oktoba 31, mwaka huu.


Tamasha hilo ambalo linatarajiwaa kufanyika Kigamboni ukiwa ni msimu wa tatu tangu kuanzishwa kwake ambapo ni mwaka 2018 na 2020, linadhaminiwa na Global TV, Championi na +255 global radio.


Akizungumza na Championi Ijumaa, Mratibu wa Singeli Festival, Masoud Kandoro alisema: “Mpaka sasa tuna wasanii 20 watakaoshiriki ambao ni Kinata MC, Balaa MC, Msaga Sumu, Man Fongo, Mzee wa Bwax.


“Meja Kunta, Dulla Makabila, Dogo Elisha, Seneta, Mimah, Vairas Mdudu, Lau Nation, Mackzube, PK MR. Konk, Six Bullet, Mczo, Morfani, Dogo Toma, Dakota mtu hatari, Nicky Nyashy na Buda Zoni,” alisema Kandoro.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic