July 27, 2013

BOBAN..
Simba imeondoka leo kwenda Tanga kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Wagosi wa Kaya, Coastal Union.

Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga amethibitisha Simba kuondoka mapema jijini Dar leo na kikosi cha wachezaji 25 kwenda Tanga kwa ajili ya mchezo huo.

Mechi hiyo itapigwa kesho kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga na Juma Nyosso na Haruna Moshi wataivaa timu yao ya zamani kwa mara ya kwanza.
NYOSSO

Boban na Nyosso wamejiunga na Coastal Union baada ya kuonyesha kutoelewana na uongozi wa Simba.

Boban aliachiwa aondoke ikionekana hana uelewano na viongozi wa Simba ambao hata hivyo hawakutoa ufafanuzi kwa nini wanamuacha.

Lakini Nyosso aliamua kuvunja mkataba mwenyewe baada ya kuona haelewani na uongozi wa Simba na haukuonyesha unataka kuendelea naye au la.

Mechi hiyo ya kesho huenda ikavuta watu wengi zaidi kutokana na wachezaji hao kucheza dhidi ya Simba.
Lakini Simba na Coastal Union zimelenga kujiimarisha zaidi kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2013-14.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic