February 8, 2020

JOHN Bocco, nahodha wa Simba amesema kuwa kilichowaponza washindwe kupata matokeo mbele ya JKT Tanzania, Uwanja wa Uhuru ni kushindwa kutumia nafasi walizozipata.

Simba ilichapwa bao 1-0 mbele ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa kwanza wa mzunguko wa pili. Bao pekee la ushindi lilifungwa na mshambuliaji Adam Adam dakika ya 24.

Bocco amesema: "Mchezo ulikuwa mgumu na wapinzani wetu walikuwa vizuri, wametengeneza nafasi moja nasi tumetengeneza nafasi tumeshindwa kuzitumia.

"Kikubwa tunashukuru kwa kuwa mchezo tumemaliza salama, tunachokifanya kwa sasa ni kujipanga kwa ajili ya mechi zetu nyingine,".

Mchezo wa kwanza wa mzunguko wa kwanza, Simba ilishinda kwa mabao 3-1, jana, Februari 7, JKT Tanzania ililipa kisasi na kusepa na pointi tatu jumla.

4 COMMENTS:

  1. Siyo kweli. Ni mbinu waliyoingia nayo JKT ya kujiaminisha mpira hauna OFFSIDE. Ata mechi zilizopita hamkustahili ushindi. Mmewadhulumu Namungo na Polisi huku mkitumia mbinu zenu chafu

    ReplyDelete
  2. Sema tu Jana kwa kuwa refa hajawabeba ndio maana mchezo ukawa mugumu.

    ReplyDelete
  3. Roho zinawauma sana eti hakuna magoli ya offside hv mechi yenu na prison kilichotokea hamkijui, mechi yenu na Lipuli kilichotokea hamkijui kama miaka miwili au mitatu mechi yenu na coastal mpaka inavunjika kilichotokea mshasau, mechi zenu na Simba mpaka Manara akaja na Tv kuwaelimisha mshasau na nyingine Ajib anafunga goli la kihalali Refa anasema offside mshasau, tumewafunga mara ngapi tukiwa pungufu uwanjani mshasau yote hayo mshasau, Malinzi alisema chini ya uongozi wake yeye Simba haitachuchukua ubingwa mshasau. Ok tatizo nishalijua wivu, roho zinawauma kweli kwa sababu mafanikio wanayopata Simba kimataifa hamuwezi kuyafikia kwa kuwa kule hakuna akina Ndolanga wala Malinzi, Eti bingwa wa kihistoria kaonyesheni huko watu wanaojua mpira ndo tutajua kweli nyie mabingwa wa kihistoria mi naona nyie mtakuwa mabingwa wa Geography, Simba medali CAF wenzetu wana medali za TFF alafu unataka kushindana na Simba, eti Simba anapulizia madawa kwani ni mara ya kwanza Al Ahly kufungwa na simba, mshasau Zamalek walichofanyiwa,Mshasau Ismailia walishapigwa (2-0)na walikuwa wanatolewa mechi ikahairishwa kwa sababu ya mvua,mshasau goli la Emmanuel Gabriel ambalo lingetupeleka nusu fainali 2003 tulipata point saba akapita Isamailia na Enyimba ndugu zetu mshawahi kupata point ngapi kwenya hatua ya makundi? au ndo nyinyi washabiki wa kwenye mitandao, As vita walivaa Mask na hawakuingia vyumbani kilichowatokea mshasau mnajisahaulisha kweli,Eti hamuwezi kupigwa tano kule mkaja kushinda hapa taifa hizo ndo fikra za watu wasioujua mpira mbona nyie mlitoka sare na RAJA Casablanca mkaenda Morocco mkapigwa sita bila (6-0) mlipuliziwa dawa nyinyi () tatizo lenu nyinyi ni wa hapa hapa FC uo ndo ukweli yani kwa kifupi mipra hamuwezi ila siasa ndo mnaiweza kwa mlianzishwa kwa madhumuni hayo ila Simba ilianzishwa na watu wa mpira hasa, mtangoja sana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic