May 2, 2015

Leo ndiyo ile mechi inayosubiriwa kwa hamu kati ya Etoile du Sahel dhidi ya mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga.


Inapigwa saa 3 usiku kwa saa za Tanzania. Na Yanga walilazimika kufanya mazoezi mepesi leo kwenye uwanja wa tenisi.

Kocha Hans van der Pluijm alitaka vijana wake kukimbia kwenye uwanja huo wa tenisi ili kupasha kidogo.
“Kuna baridi kiasi, lazima wakimbie kujiweka vizuri. Ni sawa na kupasha misuli, hakukuwa na haja ya kuanza kwenda uwanjani,” alisema Pluijm.

Mholanzi huyo amesisitiza kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho baada ya sare ya 1-1 jijini Dar es Salaam.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic