ZAHERA ATAJA MECHI SITA ZA UBINGWA YANGA
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema timu yake bado ina nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu lakini inabidi wapate ushindi katika michezo sita iliyobaki.
Zahera amesema wanahitaji kushinda michezo yote sita iliyobaki ikiwa ni dhidi ya Azam FC, Ruvu Shooting, Biashara United, Mbeya City, Tanzania Prisons na Azam FC
"Ligi bado iko wazi hakuna timu ambayo imejihakikishia ubingwa.
"Kwa upande wetu hatupaswi kufanya makosa zaidi kwenye michezo iliyobaki ili kuwa na nafasi" amesema Zahera.
Ukiondoa mchezo dhidi ya Biashara United ambao utapigwa mkoani Mara, habari njema ni kuwa michezo mingine mitano itapigwa uwanja wa Taifa
Yanga itarudi Dar kumalizia michezo yake ya nyumbani iliyobaki baada ya michuano ya AFCON ya vijana kumalizika Aprili 28 2019
Aprili 29 Yanga itaanza kampeni ya kusaka ushindi katika michezo hiyo kwa kuikabili Azam Fc katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Taifa.
Yanga ina michezo miwili dhidi ya Azam Fc na pengine mchezo huo wa April 29 utabainisha hatma ya vinara hao wa ligi katika mbio za ubingwa
Baada ya mapumziko ya Pasaka, kikosi cha Yanga kitaendelea na maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Azam FC ambao utapigwa Jumatatu ijayo
mm binafsi ni shabiki na kipenzi cha Dar Young Africans but suala la ubingwa ni less than 10% kwa timu yetu makosa n kila mechi kuruhusu goal
ReplyDeleteWewe Kocha Zahera wekeza muda mwingi kwenye mazoezi na kukisuka kikosi chako acha kutumia muda mwingi kujibizana na akina Manara, TFF na Bodi ya Ligi, acha lawamalawama....timu yako bado hairidhishi ingawa inashinda kwa taabu wakati mwingine hutoa sare na hata kufungwa....Naomba mfikishieni ujumbe huu tafadhalini
ReplyDelete