June 21, 2017Kikosi cha Singida United FC kimezidi kujiimarisha baada ya kumsajili beki Miraji Adam.

Singida United ni kati ya timu tatu zinazodhaminiwa na kampuni ya kubashiri ya SportPesa.

Miraji amesajiliwa kuongeza nguvu katika kikosi hicho kinachonolewa na Hans van der Pluijm.


Beki huyo aliyeanza kupata uzoefu akiwa na Simba, alimaliza msimu uliopita akiitumikia African Lyon ambayo imeteremka daraja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV