January 26, 2019


Licha ya jana Simba kucheza nusu fainali ya Kombe la SportPesa Supercup, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Patrick Aussems raia wa Ubelgiji ameweka wazi kuwa akili yake yote inawaza mchezo wake dhidi ya Al Ahly.

Simba inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi ambapo imepangwa kundi D sambamba na Al Ahly, As Vita na Js Saoura.

Katika kundi hill Al Ahly wanaongoza wakiwa na pointi nne wakifuatiwa na As Vita ambao wanapointi sawa na Simba inashika nafasi ya tatu kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa. 

Assuems alisema kuwa, akili yake ameilekeza kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Al Ahly kwa kuwa wanahitaji matokeo ya mazuri ili kujiwekea mazingira ya kucheza robo fainali.

“Haya mashindano tunacheza kwa sababu yapo haina jinsi, tupo kwenye wakati mgumu, tumepoteza mchezo uliopita dhidi ya As Vita ambao wenzetu walikuwa bora zaidi yetu na ukiangalia tuna mechi nyingine ngumu mbele dhidi ya Al Ahly.

“Najua haitokuwa mechi rahisi kwa sababu inahitaji maandalizi ya kutosha, nimewaambia wachezaji na wanatambua timu za Kiarabu zilivyo katika viwanja vyao vya nyumbani licha kuendelea kufuatilia wachezaji wao,” alisema Aussems

2 COMMENTS:

  1. KWAHIYO? KOCHA HUNA MBINU. VITA TULIWAZIDI UMILIKI MPIRA LAKINI WAKATUFUNGA 5 BILA WACHEZAJI WETU LEGEVU NAWEWE UNAWAANGALIA TU. HAMNA KITU KOCHA WETU UNAZIDIWA HUNA MBINU WALA HUSIKILIZI USHAURI

    ReplyDelete
  2. Chini ya huyo kocha simba haiwezi kufika mbali

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic