Wladimir Klitschko amefanikiwa
kumshinda Alexander Povetkin kwa pointi baada ya kucheza kwa raundi 12.
Hata hivyo, pambano hilo halikuwa zuri sana
kutokana na mabondia hao kutumia muda mwingi wakikumbatiana.
Ilionekana Klitschko alisoma uchezaji wa Mrusi
huyo na zaidi alikuwa anahofia ukali wa ngumi zake za kushtukiza, hivyo
akatumia muda mwingi akimkumbatia.
Pamoja na kukumbatia Klitschko alikuwa akipiga
ngumi za kushtukiza ambazo zilionekana kumwelemea Povetkin na mara nne
alishindwa kujizuia na kulamba sakafu.
Hata hivyo, baada alilalamika kwamba aliangushwa
mara mbili tu na zilizobaki alisukumwa mpinzani wake Klitschko ambaye
alimshinda kwa pointi 119-104.
0 COMMENTS:
Post a Comment