June 1, 2018


Na George Mganga

Baada ya kuenea kwa tetesi kuwa beki wa Yanga, Kelvin Yondani anahusishwa kujiunga na watani zao wa jadi Simba pamoja na Azam FC, Katibu Mkuu Yanga, Boniface Mkwasa, amefunguka.

Mkwasa ameibuka na kusema kuwa Yondani hana mipango hiyo huku akisisitiza kuwa bado wana mkataba naye hivyo ataendelea kusalia Yanga.

Katibu hiyo amesema taarifa zilizoripotiwa kuhusiana na Yondani kuondoka hazina ukweli wowote huku akieleza kuwa ni uzushi wa baadhi ya watu wanaotaka kuchaua picha ya klabu.

Wakati Mkwasa akiweka msisitizo kuwa Yondani bado ana mkataba na Yanga, uongozi wa klabu hiyo umeelezwa kuanza mazungumzo ili kumbakisha mchezaji huyo ndani ya timu.

Taarifa zinasema mara baada ya Yondani kukutana jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ndani ya Yanga, Hussein Nyika, imeelezwa walizungumza kufanya maboresho ya kuongeza mkataba ili beki huyo aendelee kusalia Yanga.

Beki huyo hajaungana na wachezaji wa kikosi cha Yanga kuelekea Kenya kwa ajili ya mashindano ya SportPesa Super Cup yanayotarajia kuanza June 3 2018 jijini Nairobi.

15 COMMENTS:

  1. NANI ALIYEKUWA AKIRIPOTI KAMA SIO WEWE MMBEA NAMBA 1 GEORGE MGANGA, halafu sijui ni mganga wa kienyeji, sasa umeona umeaibika eti unaandika baada ya kuenea taarifa kwanini usiseme BAADA YA WEWE MBEA KURIPOTI KUWA YONDANI ANAENDA SIMBA SASA ANABAKI YANGA.. YANI WE JAMAA NAKUCHUKIA HUJUI TU, NDO MATATIZO YA KUSOMA VYUO VYA ZAYONI...

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha kuendeshwa na moyo kama mwanamke,tumia akili kuliko moyo.

      Delete
    2. kweli asiendeshwe na moyo kama wewe mwanamke

      Delete
  2. pale panapokuwa na matatizo yanaandikwa mengi..lakni palipo na furaha huandiki hata kitu. Yanga ilipokuwa kwenye maandalizi ya kwenda kimataifa yaani shirikisho utakuta kataarifa kamoja tena kabaya. Mi sipendi mambo ya kifitna

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyo MGANGA WA KIENYEJI ana fitna sana , mi natamani nimjue hata kwa sura tu kitakachofanyika juu yake umbea utamwisha, na atapunguza fitna juu ya yanga, kama anatumwa ataenda kuwahadithia, hakatazwi kuandika lakini aache kupotosha

      Delete
  3. Asanteni wadau. Ila ni vema mwandishi ukatumia chanzo cha habari (source of Information), ili kuepuka kuleta mawazo ya watu badala ya habari halisi. Unajua mtandao wenu unafuatiliwa sana kwa habari za michezo.

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  4. Naamini TFF kama baba wa soka itaingilia kati hili vurugu maana haingii akilini dirisha bado halafu vurugu zinaendelea na mamlaka husika zimekaa kimya ...kule Pemba wanasema donda likikaa sana hata nzi halitaki

    ReplyDelete
    Replies
    1. RAISI WA TFF NI SIMBA, WAZIRI WA MICHEZO NI SIMBA, KWAHIYO HAYO YANAYOENDELEA HUTOSIKIA TFF IKIZUNGUMZA CHOCHOTE PA1 NA USHAURI MZURI ULIOUTOA, MAANA WOTE NDIO WANUFAIKA WAKUBWA WA MFUMO, NA NDIO MAANA KAMA ULIFATILIA VIZURI UCHAGUZI UTAGUNDUA RAIS WA TFF ALIWEKWA MADARAKANI NA BWANA MWAKI(MANGO)

      Delete
    2. wewe humjui Harrison Mwakyembe toka nasoma naye High School, ni YANGA YANGA YANGA. Nani kakudanganya kuwa Waziri wa Michezo ni Simba?

      Delete
  5. Ila niwe mwkeli Yanga kwenye usajili huwa wanakua makini sana na nakitamani sana kikosi chao kama hawatakivurga na wakakitumia kwa malengo na ikiwa wachzaji wenyewe hawataota majibu watafika mbali sana....unasajilije ukiwa na Mhilu, Maka, Akilimali na wengineo wanaochipukia vizuri?

    ReplyDelete
    Replies
    1. KAMA JINA LA TIMU LINAVYOJIELEZA NI YOUNG AFRICANS(VIJANA WA AFRIKA), NA NDIO SABABU LAZIMA VIJANA KAMA WAKINA MAKKA ,MHILU LAZIMA WAWEPO, LAKINI LAZIMA WAPATE EXPERIENCE KUTOKA KWA WACHEZAJI WAKUBWA TENA NJE YA NCHI ILI WAKUE VIZURI.

      Delete
    2. sio hao tu, yupo Mateo, kwangu mimi ndiye best player kwa chipukizi, yupo Mahadhi, yupo Ninja, yupo Kessy, hawa ni vijana kabisa huwezi kuwaacha hawa usajili nani sasa?

      Delete
  6. wewe kila siku kuleta habari za kusadikika na hasi kwa YANGA. Undishi gani unaoutumia? je una uadui na YANGA? Je unatumwa? je hakuna vilabu vingine TZ ni Yanga tu ndo unaiona kuichafua na kuleta chokochoko clubuni. Acha hayo mambo yako.

    ReplyDelete
    Replies
    1. BILA YOUNG AFRICANS HAKUNA KIKI...nani atasoma KABLOG kao bila kuandika habari za yanga, nani atanunua magazeti ya michezo ya GLOBAL PUBLISHER, bila kuweka habari za YOUNG AFRICANS..SASA WANAHITAJI KUFANYA BIASHARA NA WANAONA HAWANA HABARI ZINAZOFANYA WAUZE MAGAZETI NA WANATAMBUA HATA WASOMAJI NA WANUNUZI WAZURI WA MAGAZETI YAO NI YOUNG AFRICANS FANS, SASA WANAAMUA KUZUSHA NA KUPOTOSHA UMMA JUU YA HABARI ZA YANGA,na kwakuwa sisi tunakaa kimya basi wanaona waendeleze UJINGA wao wa kupotosha sasa hivi kila watakapokuwa wanatoa HABARI zao ni lazima tuzikosoe kama hazina ukweli.TIMU ZIPO 20 lakini wao NI YANGA TUUUUUUUU, KILA KUKICHA, KWAKUWA BILA YANGA HAKUNA KIKI..SASA KINACHOKERA ZAID NI HABARI KUPOTOSHWA NA KINA MGANGA WA KIENYEJI AMBAE HADI SHULE ALIFERI.

      Delete
  7. Kwani Mkwasi si alikuwa kocha wa taifa, kwanini baada ya Lundamili kuingia mitini kwanini hakukabidhiwa yeye timu kuiongoza?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic