April 30, 2021


 NYOTA wa West Ham United, Jesse Lingard imeelezwa kuwa hana mpango wa kurejea kwenye timu yake ya Manchester United.

 

Lingard kwa sasa anakipiga West Ham kwa mkopo tangu Januari mwaka huu, akitokea Man United na akiwa kwenye kiwango kizuri.

 

Ripoti zinaeleza kuwa Lingard anampango wa kuomba kuondoka moja kwa moja ifikapo mwishoni mwa msimu huu.

 

Tangu amejiunga na West Ham amefanikiwa kufunga mabao tisa katika mechi 11 na amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja ndani ya United.

 

West Ham wanataka kumsajili nyota huyo moja kwa moja huku ada ya kumng’oa nyota huyo ni kiasi cha pauni 15m.


 Kocha Ole Gunnar Solskjaer yupo tayari kumpokea nyota huyo kikosi kwake ilikuja kupambania nafasi yake.

 

Inaelezwa kuwa Lingard sasa ameamua kuachana na klabu yake hiyo ya utotoni, kutokana na Solskjaer kutokuwa na imani naye.

 

Mbali na West Ham, klabu kama Arsenal, Inter Milan na Paris Saint Germain zimekuwa zikimtolea macho Lingard kuelekea msimu ujao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic