Imeelezwa kuwa Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems hana papara ya usajili katika dirisha dogo ambalo linafunguliwa kesho kwa kuwataka viongozi kuweza kuchagua wachezaji makini.
Aussems amewataka viongozi wa Simba kufanya usajili wa wachezaji wawili tu ambao wamekuwa hawana mbadala ili aweze kuongeza nguvu katika ligi na michezo ya kimataifa.
"Kocha amependekeza kusajili nafasi mbili tu ambazo zipo wazi, anamtaka beki wa kulia na kiungo mkabaji hawa ndio wachezaji ambao anawataka kwenye dirisha dogo na tumejadili tumeona ni kweli hakuna mbadala wa Shomari Kapombe na Jonas Mkude hivyo lazima tufanye jambo," kilieleza.
Simba wanatarajiwa kucheza na Mbabane Swallows FC ya Swaziland katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Novemba 27 na 28 Dar es Salaam, marudio yatakuwa Desemba 3 au 4 Swaziland.
good
ReplyDeleteVZur sana
ReplyDeleteSafi sana kocha makini,kumbe una jicho la tatu....
ReplyDeletekocha tunataka na mshambuliaji wa kimataifa aliye hatar
ReplyDeleteHivi Kwel Hakuna Mbadala wa Mkude??!
ReplyDeleteHata Kotei Kwel Sio Mbadala!!