August 24, 2021


 ALIYEKUWA Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara ametambulishwa rasmi kujiunga na Klabu ya Yanga baada ya kuachana na mabosi wake wa zamani ambao kwa sasa wanaye Kaimu Ofisa Habari, Ezekiel Kamwaga.

Manara ametambulishwa leo Jumanne, Agosti 24, 2021 na uongozi wa klabu hiyo wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa mikutano wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam.

“Namshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema kwa kutujalia kukutana hapa siku ya leo katika jambo hili ambalo ni kubwa na linaloweza kutuonyesha standards ambazo tunapaswa kwenda nazo katika ufanyaji kazi.

"Mimi msemaji, nimejiunga na timu kubwa kuliko zote Afrika Mashariki na kati, tunakwenda kuchukua ubingwa, lazima tutengeneza confiedence. Nitafanya kazi zaidi ya punda mwenye njaa na kwa nguvu zaidi.

“Nimefanya kazi Simba kwa miaka takribani saba sasa kwa kadri nilivyojaliwa, huenda nilifanya vizuri kama na huenda kuna watu wamewachukizwa kwa hiki, lakini katika press yangu nilisema kama binadamu siwezi kuvumilia niliyofanyiwa.

“Wengine watasema leo Simba kesho Yanga, mimi ni professional, kama kocha au mchezaji, anaweza kwenda timu yoyote, mimi ni msemaji, nitangaze rasmi kwamba nimejiunga na klabu kubwa kuliko zote Afrika Mashariki na Kati. Huu ukubwa mnaousema ninao ni lazima nifanye kazi na klabu kubwa, klabu ambayo itanipa nafasi kushirikiana nao.

“Baada press yangu nilipotoka Simba zilikuja ofa nyingi, waliponiambia viongozi wa Yanga kwanza nilishangaa, wakaniambia sisi tunataka tufanye kazi na wewe, lakini baadae nikaona wako siriazi, sikujiuliza mara mbili.

“Mimi napenda vikombe, Yanga wakanieleza namna walivyosajili nafurahi kujiunga na klabu ambayo ninaamini itashinda kila taji msimu ujao," .

15 COMMENTS:

  1. Kwa wale wanasimba vigeu vigeu waliokuwa wakishindwa kumuelewa BARBARA... sasa watamuelewa kuwa yule Dada yupo vizuri hata MAMa Samia akimkabidhi moja ya majukumu muhimu ya kulitumia Taifa letu sitoshangaa. Kwanza kabisa jinsi Barabara alivyokuwa very proffesional katika kudili na suala la Manara haijawahi kutokea. Mpaka hii leo hatujawahi kuisikia sauti ya Barbara akizungumzia suala la Manara lakini hatimae Mungu amemjibia Barabara kwa kishindo. Asante Mungu hakika hakuna Kama wewe mweledi wa kila kitu na Mbainishaji wa haki Kati ya uongo na ukweli, Ahsante Mungu you're the greatest of all.
    Naamini kabisa katika hili la Manara, Barbara hakutendewa haki kwani wapo waliomsema vibaya wakiungana na khaji Manara na hata vyombo vya habari kadhàa vikisikika kumsema vibaya Barbara ila Manara alikuwa akihujumu simba na huo ndio ukweli na ukweli umedhihiri sasa��

    ReplyDelete
  2. Sasa ni dhahiri shahiri alikua akitumika kuhujumu upande wa pili. Njaa ni kitu kibaya sana

    ReplyDelete
  3. Leo yanga ndo timu kubwa kulko zote africa mashariki na kati??? Na Juz tu ilkuwa utopolo?? Haaa haaa

    ReplyDelete
  4. Barbra nisamehe CEO Wa mabingwa wa nchi nlikuchukulia negative juu ya hili, ila now nimekuelewa nisamehe mno Haji hutoaminika popote na shabiki yyte bora ungebak kimya ila kwa hili bro aliyekushauri kakupoteza sana

    ReplyDelete
  5. Yanga kweli bahati mbaya, leo wanamsikiluza haji akiwaita ni klabu kubwa afrika mashariki wakati hata mwezi haujapira aliwananga kuwa ni klabu duni afrika nzima? Sasa hapo nani mwenye akilikati ya manara na yanga

    ReplyDelete
  6. Utopolo wapo wengi matendo yanajionesha

    ReplyDelete
  7. Hivi ninyi Mikia wote mlizaliwa Uswahilini si mkae kimya.

    ReplyDelete
  8. Angalia mechi nyingi akiwepo Simba na yanga ni droo au yanga ishinde,asipo kuwepo Simba inamfunga yanga kirahisi tu.Huyu Yuda eskarioti

    ReplyDelete
  9. Mkizubaa hata huyo Kanji wenu (Mo) tutamchukua

    ReplyDelete
  10. Hivi mechi ya YANGA na CASABLANCA ilichezwa lini huko MOROCCO

    ReplyDelete
  11. Mpira unachezwa uwanjani na ubora wa kikosi, siyo maneno ya mtu kama yangekuwa maneno Masau Bwire angekuwa anachukua Ubingwa kila musimu,Jana mkaona MOrisson kashinda mkajifanya msajili manala ili washabiki wenu muwapoteze kweli, utopolo kazi mnayo

    ReplyDelete
  12. Subilini yanga day kwani maneno meng ya nn.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic