Uongozi wa
Shirikisho la Soka la Uganda (Fufa) umendika barua kwa Shirikisho la Soka la
Kimataifa (Fifa) kutaka kujua uhakika kuhusiana na mshambuliaji Emmanuel Okwi
kuuzwa Yanga.
Taarifa zinasema katika mtandao wa MTNfootball kwamba OKwi alijiunga na Yanga kwa kitita cha sola 100,000 lakini Fufa kupitia bosi wake, Edgar Watson imetaka kujua uhalali kuhusiana na uhamisho wake.
Fufa
kupitia Watson imetaka kujua kama ni sahihi kwa kuwa kwamba ni sahihi Okwi
aliyepelekwa SC Villa kwa mkopo akitokea Etoile du Sahel ya Tunisia kama
anaweza kucheza Yanga.
Okwi alidumu SC Villa kwa miezi miwili akiichezea timu hiyo katika Ligi Kuu ya Uganda na kufanikiwa kufunga mabao matatu.
Okwi alidumu SC Villa kwa miezi miwili akiichezea timu hiyo katika Ligi Kuu ya Uganda na kufanikiwa kufunga mabao matatu.
Lakini Mkurugenzi we SC Villa, Edgar Agaba ameiambia MTNFootball.com, Okwi alikuwa mchezaji huru kabla ya kwenda kujiunga na Yanga.
Okwi amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili na nusu na kusababisha vurugu kubwa hasa Simba wanapinga kwa kuwa wanahitaji kulipwa fedha zao dola 300,000 kutoka Etoile du Sahel.
0 COMMENTS:
Post a Comment