RONALDINHO AKIVULIWA VIATU HUKU AKIWA AMETULIA TULI |
Wachezaji
wa Raja Casablanca wametoa kali ya mwaka baada ya kumvua viatu na jezi kiungo
wa tletico Mineiro, Ronaldinho Gaucho.
Wachezaji
hao wa Raja, mara baada ya kufanikiwa kuifunga Atletico Mineiro kwa mabao 3-1 na kufanikiwa kutinga katika
fainali ya Kombe la Dunia la klabu, wakamvamia Ronaldinho.
Ronaldinho
ndiye aliyefunga bao pekee la Atletico Mineiro kwa mkwaju wa adhabu, wakati
anashangaa, mmoja wao alimuomba jezi akampa.
Lakini
mara viongozi, wachezaji wakamvamia na kuanza kugombea kukumkumbatia kabla ya
wengine kuinama na kumvua viatu.
Wengine
walikuwa wanalazimisha kumkumbatia muda mwingi zaidi zaidi huku wakisubiri.
Raja sasa itacheza fainali dhidi ya Mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich ya Ujerumani.
0 COMMENTS:
Post a Comment