April 16, 2014

AWADHI (MWENYE MPIRA) AKIWA MAZOEZINI
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Awadh Juma, amesema bado analikumbuka bao lake alilomfunga kipa Juma Kaseja kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe lakini amewaonya Yanga kuwa hata wakibadilisha kipa atahakikisha anamtungua.



Awadh alisajiliwa na Simba kwenye usajili wa dirisha dogo akitokea Mtibwa Sugar ambapo katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Yanga, alifunga bao jepesi baada ya kumnyang’anya Kaseja mpira na kuutupia wavuni, jambo ambalo liliwauma mashabiki wa klabu hiyo iliyolala kwa mabao 3-1.

Yanga na Simba zinatarajiwa kukutana Jumamosi ya wiki hii kwenye mechi ya mwisho ya ligi kuu ambayo tayari bingwa amepatikana, ambaye ni Azam FC, lakini Awadh anatamani Yanga wampange tena Kaseja.

 Awadh amesema bado analikumbuka bao hilo na amejipanga kuhakikisha anapeleka tena kilio Jangwani kwani anaamini wana kikosi bora lakini matatizo ya hapa na pale yamesababisha wafanye vibaya msimu huu.
 “Ni mechi ngumu lakini sisi tumejipanga kuhakikisha tunashinda tu. Yah! Nakumbuka lile bao dhidi ya Kaseja bado ni zuri. Makipa wote wa Yanga ni wazuri lakini nimejipanga kuhakikisha namtungua mtu huyo Jumamosi ingawa angekaa Kaseja ingekuwa poa zaidi,” alisema Awadh.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic