Kocha wa
Simba, Zdravko Logarusic amesema anatamani mechi ya Simba na Yanga ipigwe usiku
kwa kuwa ndiyo muda mzuri kwake.
Kocha huyo
amesema kwa sasa ana furaha kubwa kwa kuwa jijini Dar es Salaam kuna hali ya
baridi na mvua, lakini furaha yake itatimia kama mechi hiyo itapigwa usiku
kwani ndiyo muda wake muafaka.
Mechi ya
Yanga dhidi ya Simba inatarajiwa kupigwa Jumamosi hii majira ya saa 10 jioni kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Loga alisema anatamani mechi hiyo ingebadilishwa muda na
ingekuwa usiku ingekuwa na faida kubwa sana kwake.
“Hii mechi
ingepigwa usiku ingekuwa safi sana kwa sababu ingekuwa na faida nyingi, kwa
watazamaji na hata kwangu pia; kwanza ingekuwa usiku wa saa moja hivi ingekuwa
nafuu kwa wafanyakazi kupata muda wa kupumzika na kujiandaa kuja kwenye mechi.
“Najua hii
mechi ni kubwa na kila mmoja angependa kuishuhudia na siku kama ya Jumamosi
watu wengi wanaenda kazini na kufanya kazi kwa saa chache, hivyo ingewekwa
usiku ingetoa muda mzuri kwa watu wote kuishuhudia.
“Halafu
hata kwangu pia, ingekuwa safi kwani huwa napata shida muda wa mchana au jioni
kutokana na kusikia sana joto na kutokwa jasho muda mwingi lakini hii hali ya
hewa ya siku hizi mbili tatu imekuwa nzuri kwangu na hasa wakati wa usiku ndiyo
huwa safi kabisa, natamani TFF waipeleke mechi hii ya Yanga na Simba wakati wa
usiku.
“Kwa hiyo
ingekuwa usiku mambo yangekuwa safi, lakini hili la usiku linawezekana kwa
sababu uwanja una kila kitu kwa ajili ya giza, zipo taa kubwa na zenye mwanga
wa kutosha halafu pia hata waandishi watafaidika na picha wanazopiga, huwa
zinatoka safi wakati wa usiku na mahali penye mwanga kama pale uwanjani,”
alisema kocha huyo mzungumzaji sana.
0 COMMENTS:
Post a Comment