HALL (KUSHOTO) WAKATI AKIWA AZAM |
Viongozi na
wachezaji wa timu ya Azam FC wametoa shukrani kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo,
Stewart Hall, kwa kuchangia mafanikio ya timu hiyo na kuweza kuibuka mabingwa
wa Ligi Kuu Bara.
Hall
aliifundisha timu hiyo katika mzunguko wa kwanza na mpaka anaiacha ilikuwa
haijawahi kupoteza mchezo.
Akizungumza
na Championi Jumatano, Hall alisema amefurahi kwa kiasi kikubwa timu hiyo
kuweza kuleta mabadiliko huku wachezaji pamoja na viongozi wa timu wakiwa
wamempigia simu kumshukuru kwa mchango wake.
Stewart
alisema mabadiliko yaliyotokea safari hii katika soka ni mazuri na ndiyo
yatafanya soka la Tanzania kuendelea kukua kwa kiasi kikubwa kutokana na
changamoto na zama za Simba na Yanga huenda zikatoweka.
“Nina
furaha sana kutokana na Azam kutwaa ubingwa msimu huu, haya ndiyo mabadiliko
tuliyokuwa tunayahitaji na nimepata meseji za shukrani kutoka kwa viongozi kama
Bakhresa, Kali Ongalla na wengine wengi.
“Lakini
kikubwa hapa ni mabadiliko kwa kiasi kikubwa, msimu huu tumeona changamoto
nyingi sana kutoka kwa timu nyingi ili kumaliza zama za Simba na Yanga. Kwa
sasa wanasoka wameamua kuleta mabadiliko makubwa, tofauti na zamani,” alisema
Hall.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment