AWADHI (MWENYE MPIRA) AKIWA MAZOEZINI |
Awadh
alisajiliwa na Simba kwenye usajili wa dirisha dogo akitokea Mtibwa Sugar
ambapo katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Yanga, alifunga bao jepesi baada
ya kumnyang’anya Kaseja mpira na kuutupia wavuni, jambo ambalo liliwauma
mashabiki wa klabu hiyo iliyolala kwa mabao 3-1.
Yanga na
Simba zinatarajiwa kukutana Jumamosi ya wiki hii kwenye mechi ya mwisho ya ligi
kuu ambayo tayari bingwa amepatikana, ambaye ni Azam FC, lakini Awadh anatamani
Yanga wampange tena Kaseja.
Awadh amesema bado analikumbuka bao hilo na amejipanga
kuhakikisha anapeleka tena kilio Jangwani kwani anaamini wana kikosi bora
lakini matatizo ya hapa na pale yamesababisha wafanye vibaya msimu huu.
“Ni mechi ngumu lakini sisi tumejipanga
kuhakikisha tunashinda tu. Yah! Nakumbuka lile bao dhidi ya Kaseja bado ni
zuri. Makipa wote wa Yanga ni wazuri lakini nimejipanga kuhakikisha namtungua
mtu huyo Jumamosi ingawa angekaa Kaseja ingekuwa poa zaidi,” alisema Awadh.
0 COMMENTS:
Post a Comment