April 24, 2014


Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic ameshindwa kuficha hisia zake kwa Miss Tanzania 206, Wema Sepetu.

Logarusic raia wa Croatia amesema pamoja na kuwa mrembo lakini Wema ni mcheshi sana, jambo lililomvutia.

“Hana maringo na hicho ndiyo kitu kizuri, ingawa nimekutana naye kwa mara ya kwanza lakini utafikiri tunafahamiana.
“Kipimo kizuri cha ubinadamu ni kuonyesha unaweza kuwajali watu.
“Nimezungumza vizuri na Wema, ningependa niendelee kuwasiliana naye,” alisema Logarusic na alipoulizwa kama angependa hata kuwa na uhusiano zaidi ya hapo, akajibu.

“Aah, huko kwingine ingawa kuwa na urafiki na mrembo kama Wema, si jambo baya. Najuana na warembo wengi tu nao ni rafiki zangu.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic