Pamoja
na kuwa na umbo zuri, fedha za kutosha mwanadada maarufu, Kim Kardashian
ameonekana kuwashangaza wengi kutokana na kuvaa sketi na blausi iliyoonekana
kutokuwa nzuri.
Kim
,33, alionekana akiwa amevaa sketi hiyo iliyotengenezwa kwa ngozi, lakini
haikuwa na mvuto na kusababisha watu wengi kushangazwa na hilo.
Picha
nyingi za mwanadada huyo mpenzi wa msanii maarufu wa hip hop wa Marekani, Kanye
West zimepondwa kwamba alivaa gauni la kubahatisha.
Wengine
wameeleza kwamba kuvaa nguo za bei kubwa, haina maana ndiyo lazima upendeze,
badala yake ni jinsi ya kujipangilia na kujitambua ulivyo.
'
0 COMMENTS:
Post a Comment