Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic ameshindwa kuficha
hisia zake kwa Miss Tanzania 206, Wema Sepetu.
Logarusic raia wa Croatia amesema pamoja na kuwa mrembo
lakini Wema ni mcheshi sana, jambo lililomvutia.
“Hana maringo na hicho ndiyo kitu kizuri, ingawa
nimekutana naye kwa mara ya kwanza lakini utafikiri tunafahamiana.
“Kipimo kizuri cha ubinadamu ni kuonyesha unaweza
kuwajali watu.
“Nimezungumza vizuri na Wema, ningependa niendelee
kuwasiliana naye,” alisema Logarusic na alipoulizwa kama angependa hata kuwa na
uhusiano zaidi ya hapo, akajibu.
“Aah, huko kwingine ingawa kuwa na urafiki na mrembo
kama Wema, si jambo baya. Najuana na warembo wengi tu nao ni rafiki zangu.”
0 COMMENTS:
Post a Comment