April 19, 2014


Mshambuliaji wa Simba, Betram Mwombeki, ameifungia vioo klabu yake ya Simba na kuamua kufanya mambo yake kwa sasa kutokana  na kutokuwa na nafasi katika kikosi cha kocha mkuu wa timu hiyo, Mcroatia, Zdravko Logarusic.


Mwombeki ambaye alipata kutamba sana mwanzoni mwa msimu huu wakati timu hiyo ikiwa chini ya kocha Abdallah Kibadeni, amekuwa na wakati mgumu tangu kikosi hicho kiwe chini ya Logarusic.

Mwombeki amesema kwa sasa yupo nyumbani anafanya shughuli zake kwa ajili ya maisha yake ya baadaye.
Alisema kuhusiana na sababu za kutoonekana katika kikosi cha timu hiyo, hawezi kuzizungumza kwa sasa lakini atafanya hivyo muda utakapofika, ikiwa ni pamoja na hatma yake ndani ya klabu hiyo.
 “Haya ni mambo yangu binafsi, hivyo siwezi kuyazungumza kwa sasa lakini muda ukifika nitazungumza na kila mtu atajua nini hatma yangu katika kikosi cha Simba.
“Hivi sasa sionekani Simba kutokana na sababu mbalimbali lakini kubwa zaidi ni kwamba nilikuwa naumwa ila sasa naendelea vizuri, pia kuna baadhi ya mambo yangu binafsi ninafanya,” alisema Mwombeki.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic