April 23, 2014

Real Madrid imeibuka na ushindi wa bao 1-0 katika nusu fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich katika mechi iliyomalizika hivi punde.

Katika mechi hiyo kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid, wenye walipata bao lao katika dakika ya 19, mfungaji akiwa Karim Benzema aliyemalizia krosi ya chini ya Daniel Carvajal.
Baadaye Madrid ilipoteza nafasi za kufunga kupitia Cristiano Ronaldo na Angelo Di Maria.
Hata hivyo, Bayern ambao ni mabingwa watetezi, waliwaonyesha kazi Madrid ambao walikuwa wakitafuta mpira kwa tochi.
Madrid walitumia muda mwingi kujilinda huku wakifanya mashambulizi ya kushitukiza.
Lakini Bayern wanaonolewa na Pep Guardiola ndiyo wakatawala huku wakipiga pasi fupifupi.


Real Madrid: Casillas, Carvajal, Sergio Ramos, Pepe (Varane 73), Fabio Coentrao, Modric, Alonso, Di Maria, Isco (Ilarramend 83), Benzema, Ronaldo(Bale 73).
Subs: Diego Lopez, Varane, Bale, Marcelo, Casemiro, Morata, Illarramendi.
Booked: Isco.
Goal: Benzema 19.

Bayern Munich: Neuer, Rafinha (Javi Martinez 66), Boateng, Dante, Alaba, Lahm, Schweinsteiger (Muller 74), Robben, Kroos, Ribery (Gotze 72), Mandzukic.
Subs: Zingerle, Pizarro, Weiser, Muller, Raeder.
Referee: Howard Webb (England)














0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic