Real Madrid
imeibuka na ushindi wa bao 1-0 katika nusu fainali ya kwanza ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich katika mechi iliyomalizika hivi punde.
Katika mechi
hiyo kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid, wenye walipata bao lao
katika dakika ya 19, mfungaji akiwa Karim Benzema aliyemalizia krosi ya chini
ya Daniel Carvajal.
Baadaye
Madrid ilipoteza nafasi za kufunga kupitia Cristiano Ronaldo na Angelo Di
Maria.
Hata hivyo,
Bayern ambao ni mabingwa watetezi, waliwaonyesha kazi Madrid ambao walikuwa
wakitafuta mpira kwa tochi.
Madrid
walitumia muda mwingi kujilinda huku wakifanya mashambulizi ya kushitukiza.
Lakini
Bayern wanaonolewa na Pep Guardiola ndiyo wakatawala huku wakipiga pasi
fupifupi.
Real
Madrid: Casillas, Carvajal, Sergio Ramos, Pepe (Varane 73), Fabio Coentrao, Modric,
Alonso, Di Maria, Isco (Ilarramend 83), Benzema, Ronaldo(Bale 73).
Subs: Diego Lopez, Varane, Bale, Marcelo, Casemiro, Morata, Illarramendi.
Subs: Diego Lopez, Varane, Bale, Marcelo, Casemiro, Morata, Illarramendi.
Booked:
Isco.
Goal:
Benzema 19.
Bayern
Munich: Neuer, Rafinha (Javi Martinez 66), Boateng, Dante, Alaba, Lahm,
Schweinsteiger (Muller 74), Robben, Kroos, Ribery (Gotze 72), Mandzukic.
Subs: Zingerle, Pizarro, Weiser, Muller, Raeder.
Subs: Zingerle, Pizarro, Weiser, Muller, Raeder.
Referee: Howard Webb (England)
0 COMMENTS:
Post a Comment