Timu ya Taifa ya Burundi (Intamba Mu
Rugamba) inatarajiwa kuwasili nchini kesho (Aprili 24 mwaka huu) saa 12 jioni
kwa ndege ya Kenya Airways tayari kwa mechi dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa
Jumamosi (Aprili 26 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Intamba Mu Rugamba itakuwa na msafara
wa watu 28 wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi, na itafikia hoteli
ya Accomondia. Mechi hiyo itachezwa kuanzia saa 10 jioni.
Nayo Taifa Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager ipo kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach
ikijiandaa kwa mechi hiyo itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Kenya.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa
sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa VIP A kiingilio
kitakuwa sh. 20,000 wakati VIP B na C ni sh. 10,000. Mechi hiyo ni sehemu ya
maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
0 COMMENTS:
Post a Comment