July 9, 2014


 
BAADHI YA WAPIGAPICHA WA AZAM TV (SI HAWA WALIOONDOLEWA MAZOEZINI YANGA) WAKIWA KATIKA MAJUKUMU YAO KWENYE UWANJA WA AZAM COMPLEX, CHAMAZI JIJINI DAR ES SALAAM. UWANJA HUU UNAMILIKIWA NA AZAM FC

Waandishi na wapiga picha wa Azam TV leo wameondolewa kwenye mazoezi ya Yanga yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola, Mabibo jijini Dar es Salaam.
Waandishi hao waliondolewa baada ya kuanza kurekodi kazi alizokuwa akifanya Kocha Mkuu, Marcio Maximo.


Yanga walikuwa wakiendelea na mazoezi chini ya kocha huyo raia wa Brazil, lakini baadaye meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh alikwenda na kuwaomba watoke nje.

Ingawa Hafidhi hakutaka kulizungumzia suala hilo, imeelezwa Yanga walipata ‘magutu’ kwamba huenda Azam TV wanarekodi mafunzo ya Yanga na baadaye watatoa nafasi kwa kikosi cha Azam FC ambao ni ndugu zao kuzitumia kwenye mambo yao ya ufundi.

Hivyo wakaona ni jambo la msingi Azam TV kutopewa nafasi ya kurekodi mazoezi hayo ya Yanga ambayo yanaendelea chini ya Maximo.

Hafidhi aliwafuata waandishi hao kistaarabu na kuwaeleza uamuzi wa uongozi wa klabu yake, nao wakatii bila ya ubishi na kuondoka eneo hilo.

Yanga na Azam TV zimekuwa na upinzani mkali hasa baada ya uongozi wa Yanga kuanza kupinga kampuni hiyo kuonyesha mechi zao licha ya kulipa fedha Sh milioni 100 ambazo ni chache.

Lakini Azam TV imekuwa ikiendelea kuonyesha kwa kuwa imeingia mkataba na bodi ya ligi ambayo inasisitiza hivyo ni sahihi.

Mara kadhaa, mashabiki wa Yanga wamekuwa wakiagiza kamera za Azam TV kuondolewa wakati wa mechi za Ligi Kuu Bara zinazoihusu Yanga.

.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic