Kipigo cha mabao 7-1 walichokipata Brazil kutoka kwa
Ujerumani katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia kimewashitua wapenda
soka wengi duniani.
Lakini kwa uhalisia, Ujerumani ilionekana itashinda
kutokana na kuwa na kikosi imara zaidi ya Brazil.
SALEHJEMBE alibashiri kuwa Brazil italala kwa mabao
4-0, lakini akakosea, kumbe ni 7-1 ambazo ni nyingi sana na zinasikitisha.
Pamoja na vurugu katika sehemu za nchi hiyo, kikubwa
ambacho kimeonekana kwa Wabrazil hao ni machozi yao kwa nchi yao.
Wengi wamelia kuanzia uwanjani, barabarani na kila
sehemu wakionyesha kuumizwa na kilichotokea kwa timu yao.
Lakini vilio vimeonyesha kutojali ni nani analia,
mtoto, awe wa kike au wakiume, wasichana na wavulana lakini wanaume na
wanawake.
Wote wamelia, tena si vilio vya kutunga, badala yake
ni vile vinavyoonyesha wazi wana uchungu na nchi yao.
Kweli kuna wakati walifika wakaizomea timu yao kwa
nguvu, wana haki wa kuwa waliumia na hawkautegemea kipigo hicho kikubwa kuwahi
kutokea kwao na kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia.
Sasa wenyeji ndiyo imekuwa timu iliyopata kipigo
kikali kuliko hata zile timu zilizoonekana ni vibonde kutoa Asia na Afrika.
Wana haki ya kulia, machozi yao ni uzalendo. Lakini jiulize,
kama Taifa Stars ingepoteza kwa idadi hiyo mbele ya mashabiki 60,000, kungekuwa
hata na mmoja ambaye angeangua kilio?
|
0 COMMENTS:
Post a Comment