July 9, 2014



Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesogeza Ligi Kuu Bara kwa mwezi mmoja zaidi.
Awali ligi hiyo ilipangwa kuanza Agosti 24, lakini sasa taarifa zinaeleza ligi hiyo itaanza Septemba 20.

Habari za uhakika kutoka ndani ya TFF zinaeleza tayari barua za uamuzi huo wa TFF kwenda kwa klabu za ligi hiyo zimeanza kupelekwa.
Hata hivyo taarifa hizo zimeonyesha kuwashtua wengi kama kweli TFF wako siriaz au wanatania katika jambo hilo.
Maana moja ya sababu zilizoelezwa ni kuipisha michuano ya Kombe la Kagame itakayofanyika nchini Rwanda kuanzia mwezi ujao na itakuwa ni ya wiki mbili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic