September 23, 2014


Pamoja na kuanza kwa kupoteza mechi ya kwanza, Stand United bado ina matumaini ya kuinuka na kufanya vema.

Kocha wake msaidizi, Athumani Bilal amesema wanaweza kubadilika na kufanya vizuri kwa kuwa wameona makosa yao.
“Kweli tumeumua sana kutokana na kipigo kikubwa tena nyumbani. Tumeanza kuyafanyia kazi makosa.
“Tunaamini tutajirekebisha na kufanya vema katika mechi zinazokuja.
“Hakuna sababu ya kukata tamaa na tunawaambia mashabiki waendelee kutuunga mkono,” alisema Bilal maarufu kama Bilo.
Stand United ikiwa kwenye Uwanja wake wa nyumbani ilikutana na kipigo cha mabao 4-1 dhidi ya Ndanda FC ambayo pia imepanda daraja msimu huu.
Hiyo ilikuwa ni mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ambayo imeitupa timu hiyo mkiani.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic