Mkosi! Simba itacheza mechi yake ya Oktoba
12 bila ya mshambuliaji wake Paul Kiongera.
Vipimo vilivyotolewa leo kwenye hospitali ya
rufaa ya Muhimbili vimeeleza Kiongera ameumia sana goti lake na tayari
imepitishwa apumzike wiki sita.
Hali hiyo imejulikana baada ya daktari wa
Simba kusafiri na Kiongera hadi Dar es Salaam wakitoka kambini Zanzibar na
kufanyiwa vipimo.
Kiongera aliingia kwenye mechi dhidi ya
Coastal Union kuchukua nafasi ya Amissi Tambwe, lakini akatoka ikiwa imebaki
dakika moja na nafasi ya kuchukuliwa na Kiemba ambaye hakugusa hata mpira.
Majeruhi wengine ni Haruna Chanongo ambaye
amebakiza siku mbili kabla ya kurudi uwajani na kuanza mazoezi mepesi na Issa
Rashid maarufu kama Baba Ubaya.
0 COMMENTS:
Post a Comment