Nyuki bana, nao wana yao. Katika mechi ya
Ligi Kuu Bara, Jumapili iliyopita wakati Mtibwa Sugar ikiivaa Yanga,
waliwakimbiza wachezaji wa Mtibwa.
Wachezaji hao walikuwa wanashangilia bao
lililofungwa na mwenzao Mussa Hassan Mgosi, ghafla nyuki hao wakaibuka na
wachezaji hao wakalazimika kutimua mbio.
Cameraman wa Azam FC na mwenzake, pia
walilazimika kuacha kazi yao na kutimua mbio baada ya lundo hilo la nyuki
kuungana nao wakati wakishangilia.
Hata hivyo halikuwa tukio la muda mrefu,
nyuki hao ‘walichukua za time’.
Mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara iliisha kwa
Mtibwa Sugar kushinda kwa mabao 2-0 kwenye uwanja wa Jamhuri.
0 COMMENTS:
Post a Comment