Pamoja na kuanza kwa kupoteza mechi ya
kwanza, Stand United bado ina matumaini ya kuinuka na kufanya vema.
Kocha wake msaidizi, Athumani Bilal amesema
wanaweza kubadilika na kufanya vizuri kwa kuwa wameona makosa yao.
“Kweli tumeumua sana kutokana na kipigo
kikubwa tena nyumbani. Tumeanza kuyafanyia kazi makosa.
“Tunaamini tutajirekebisha na kufanya vema
katika mechi zinazokuja.
“Hakuna sababu ya kukata tamaa na
tunawaambia mashabiki waendelee kutuunga mkono,” alisema Bilal maarufu kama
Bilo.
Stand United ikiwa kwenye Uwanja wake wa
nyumbani ilikutana na kipigo cha mabao 4-1 dhidi ya Ndanda FC ambayo pia
imepanda daraja msimu huu.
Hiyo ilikuwa ni mechi ya ufunguzi wa Ligi
Kuu ambayo imeitupa timu hiyo mkiani.
0 COMMENTS:
Post a Comment