October 21, 2014


Adel Taarabt ameibuka na kujibu mapigo kwa kocha wa QPR, Harry Redknapp na kusema hampendi.
Kocha huyo alisema Taarabt ni mvivu na ameongezeka kilo tatu.

Akasisitiza hawezi kutoa nafasi kwa mchezaji mzembe ambaye analipwa pauni 70,000 kwa wiki.
Taarabt amesema amekuwa akishangazwa na kocha huyo Mwingereza kumyima nafasi.
Pia amemkumbusha kwamba akiwa AC Milan aliwaweka benchi Robinho na Kaka.
Halafu akafungua fulana mbele ya waandishi na kuonyesha tumbo lake kuonyesha si kweli kwamba ana kitambi.

Watu wamekuwa wakihoji kutokana na Redknapp, mmoja wa makocha wakongwe England kushindwa kumtumia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic