Yule mshambuliaji wa timu
ya taifa ya Benin aliyeshindwa kufurukuta mbele ya mabeki Nadir Haroub ‘Cannavaro’
na Kelvin Yondani jana amepiga bonge la bao akiichezea timu yake dhidi ya
Manchester United.
Stephane Sessegnon amefunga
bao hilo kwa shuti kali la kasi ya kilomita 91 kwa saa na kuifanya West Bwrom
iongoze kwa bao moja dhidi ya Man United.
Mshambuliaji huyo alitua
jijini Dar es Salaam na kuingoza Benin iliyotandikwa kwa mabao 4-0 dhidi ya
Taifa Stars.
Bao lake lilikuwa moja ya
mabao manne bora kwenye mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya bao 2-2.
0 COMMENTS:
Post a Comment