Adel Taarabt ameibuka na
kujibu mapigo kwa kocha wa QPR, Harry Redknapp na kusema hampendi.
Kocha huyo alisema Taarabt
ni mvivu na ameongezeka kilo tatu.
Akasisitiza hawezi kutoa
nafasi kwa mchezaji mzembe ambaye analipwa pauni 70,000 kwa wiki.
Taarabt amesema amekuwa
akishangazwa na kocha huyo Mwingereza kumyima nafasi.
Pia amemkumbusha kwamba
akiwa AC Milan aliwaweka benchi Robinho na Kaka.
Halafu akafungua fulana
mbele ya waandishi na kuonyesha tumbo lake kuonyesha si kweli kwamba ana
kitambi.
Watu wamekuwa wakihoji
kutokana na Redknapp, mmoja wa makocha wakongwe England kushindwa kumtumia.
0 COMMENTS:
Post a Comment