April 2, 2015

MBEYA CITY WATAKUWA UGENINI MJINI MTWARA.
Ligi Kuu Bara inatarajiwa kendelea kutimua vumbi mwishoni mwa wiki katika sita nchini, kwa michezo minne kucheza siku ya jumamosi na michezo mwiwili kuchezwa siku ya jumapili.


Jumamosi uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Simba SC kutoka jijini Dar es salaam, huku jijini Tanga Coastal Union wakiwakaribisha maafande wa jeshi la Magereza nchini Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Ndanda FC ya Mtwara watakuwa wenyeji wa wagonga nyundo timu ya Mbeya City katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, wakati maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa Ruvu Shooting wakicheza na ndugu zao JKT Ruvu katika uwanja wa Mabatin uliopo Mlandizi.

Siku ya jumapili Stand United watawakaribisha wakata miwa kutoka Morogoro Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Kambarage, huku Mgambo Shooting wakiwa wenyeji wa timu ya  Polisi Morogoro kwenye uwanja wa Mkwakani jijini Tanga.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic