Rais wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewatakia kila la
kheri wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika
(CC) Young Africans, katika mchezo wa marudiano dhidi ya FC Platinum ya
Zimbabwe utakochezwa siku ya jumamosi kwenye uwanja Mandava uliopo Gweru
Bulawayo.
Malinzi
amesema Young Africans hawapaswi kubweteka na ushindi walioupata awali wa mabao
5-1, kikubwa wanapaswa kwenda kupambana kusaka ushindi ugenini ili kuweza
kufuzu kwa hatua inayofuata ya timu 16.
Endapo Young
Africans itafanikiwa kuwatoa FC Platinum itaingia katika hatua ya 16 bora na
itakutana na mshindi kati ya timu za Benifica de Luanda ya Angola au Etoile du
Saleh ya Tunisia.
0 COMMENTS:
Post a Comment