Yanga imetua salama salimini nchini Tunisia kwa ajili ya mechi yake ya pili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Etoile du Sahel.
Kama kawaida, vituko kadhaa kutoka kwa Waraabu kwa leongo la kuwachosha, vilifanyika katika Uwanja wa Ndege wa Tunis.
Lakini Yanga walionekana kujiandaa na tayari wamepanda basi kuanza safari ya kwenda Sousse.
Sousse ndiyo mji ambao mechi kati ya Yanga dhidi Etoile itachezwa.
Yanga inaivaa Etoile kesho
katika mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho. Mechi ya kwanza iliisha kwa sare ya 1-1 jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment