Beki Nadir Haroub Cannavaro
ambaye ni nahodha wa Yanga amesema
watapambana hadi mwisho.
Cannavaro amesema hayo
akiwa tayari ndani ya ndege kwa safari ya kwenda nchini Tunisia kuivaa Etoile
du Sahel.
Cannavaro ana kumbukumbu ya
Tunisia, mara ya mwisho aliichezea Yanga nchini humo na kufungwa kwa mabao 3-0
dhidi ya Esperance.
“Kazi itakuwa ngumu, lakini
tutapambana vilivyo ndugu yangu,” alisema.
Yanga inaivaa Etoile kesho
katika mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho.
0 COMMENTS:
Post a Comment