May 26, 2015

 
HAJI MWINYI AKISAINI MKATABA KUICHEZEA YANGA, LEO MBELE YA MENEJA WA YANGA, HAFIDH SALEH.
Yanga imefanikiwa kumsajili beki Haji Mwinyi kutoka KMKM ya Zanzibar.


Haji Mwinyi amesaini kuichezea Yanga leo na sasa yuko njiani kurejea kwa Zanzibar.

“Kweli Haji amesaini Yanga leo, ataichezea kwa miaka miwili na kila kitu kimeisha.

“Tuko njiani tunarejea Zanzibar, shughuli zote zimefanyika kwenye makao makuu ya Yanga,” kilieleza chanzo.

Mwinyi alikuwa katika kikosi cha Taifa Stars kilichoshiriki michuano ya Kombe la Cosafa nchini Afrika Kusini.

Pamoja na Mwinyi, Yanga imefanikiwa kumnasa kipa wa Kagera Sugar, Benedicto Tinocco.

Tinocco licha ya kuwa tegemeo katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana, pia aliwahi kuwa kipa bora wa michuano ya Copa Coca Cola.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic