Yanga
imefanikiwa kumsajili beki Haji Mwinyi kutoka KMKM ya Zanzibar.
Haji
Mwinyi amesaini kuichezea Yanga leo na sasa yuko njiani kurejea kwa Zanzibar.
“Kweli
Haji amesaini Yanga leo, ataichezea kwa miaka miwili na kila kitu kimeisha.
“Tuko
njiani tunarejea Zanzibar, shughuli zote zimefanyika kwenye makao makuu ya
Yanga,” kilieleza chanzo.
Mwinyi
alikuwa katika kikosi cha Taifa Stars kilichoshiriki michuano ya Kombe la
Cosafa nchini Afrika Kusini.
Pamoja
na Mwinyi, Yanga imefanikiwa kumnasa kipa wa Kagera Sugar, Benedicto Tinocco.
Tinocco
licha ya kuwa tegemeo katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana, pia aliwahi
kuwa kipa bora wa michuano ya Copa Coca Cola.
0 COMMENTS:
Post a Comment