June 22, 2016





Wakati TP Mazembe inajiandaa kuja jijini Dar es Salaam kucheza na Yanga, mmiliki wake Moise Katumbi Chapwe amehukumiwa kwenda jela.



Chapwe ,51, aliyeondoka nchini DR Congo mwezi Mei, mwaka huu kwenda Ulaya, amehukumiwa kwenda jela miezi 36.


Katumbi ambaye yuko nje ya DR Congo, amepatikana na hatia ya kuuza moja ya mali zake katika eneo la Lubumbashi ikionekana hakufuata sheria za nchi hiyo huku akijua ni makosa.

Hata hivyo, tajiri huyo ambaye alihukumiwa bila kuwepo mahakamani, inaonekana ameingia kwenye tatizo hilo baada ya uamuzi wake wa kuamua kugombea urais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya DR Congo.


Uamuzi huo unaonekana kumkera Rais Joseph Kabila aliye madarakani tokea mwaka 2001 ameamua kuendelea kugombea uongozi tena licha ya kujua anavunja katiba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic