September 20, 2021


 NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amekuwa akipasua kichwa namna ya kuweza kutatua tatizo la mabao ya mipira iliyokufa jambo ambalo limekuwa tatizo kwa timu hiyo kwa hivi karibuni.


Jana Yanga ilipoteza kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers Niger na kumaliza mwendo katika hatua ya awali.

Ni safu ya ulinzi pamoja na viungo wa Yanga walikuwa wamekaa kikao ili kujadili namna ya kuweza kuondoa hali hiyo ya kufungwa mabao kwa mipira ya adhabu.


Taarifa kutoka kwa moja ya viongozi wa Yanga ilieleza kuwa Nabi hafurahishwi na kuona timu hiyo inafungwa mabao yanayotokana na mipira ya kutengwa jambo ambalo linampasua kichwa.


"Baada ya mchezo dhidi ya Rivers United lile bao lilifanya Nabi aweze kukaa na wachezaji na kuzungumza nao kuhusu makosa ya mara kwa mara, kikubwa anahitaji umakini na hilo litakuwa na mabadiliko makubwa," amesema mtoa taarifa hiyo.


Moja ya mabeki wa kutegemewa ndani ya Yanga ambaye ni nahodha, Bakari Mwamnyeto alisema kuwa kumekuwa na tatizo katika mabao wanayofungwa kutokana na mipira ya kutengwa jambo wanalolinfanyia kazi ili lisijirudie.


"Makosa kwa upande wa mabao ambayo tunafungwa ikiwa ni yale ya kona na faulo ni moja ya mambo ambayo hatupendi kuona yanatokeo hivyo kwa wakati huu tunazidi kujiweka sawa ili kupunguza makosa,". 


Mchezo ujao wa Yanga ni dhidi ya Simba ambao ni maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa ligi unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 25.

14 COMMENTS:

  1. Tazama namna nabi aluvokuwa kocha muanifu na sio katika wale wanaolalamika kila kukicha kuwa wanaonewa. Yeye hata siku moja hatujawahi kumsikia kulalamika na hata ile ya kuwa wamesingiziwa korona

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyo ni professional sio mwanasiasa yanga ni timu ya siasa ndo mana wanssajili wanasiasa badala ya wachezaji wakamsajili manara akawaminisha eti atafanya kila juhudi yanga inaingia group stage mashindano ya CAF yako wapi utafikiri ndo kocha yy na ndo mchezaji yy siasa tupu

      Delete
    2. Siasa Maana yake nini ???

      Delete
  2. huyo mwamnyeto akae benchi YANGA

    ReplyDelete
  3. Mwamnyeto hafuati mipira inayopigwa golini. Mpira ukipigwa golini lazima walinzi waufuate na sio kingoja washambuliaji wafuate ndio wakabe.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shida sio mipira ya kufa shida Ni pale unApokutana Na Kipaji ZAIDI Maarifa yanatakiwa yaongezeke .YANGA hawajaanza Leo kufungwa .KIGOMA walifungwa YANGA. Kombe la kagame YANGA hao hao wakafungwa mapema.Kwa Mkapa Na Rivers United YANGA hao wamefungwa tena .Wanaenda Nigeria nako wanafungwa tena !
      Halafu viongozi hawana Maarifa Na kuona mbali kwasababu Baada ya kufungwa Na Rivers United wangeenda kwa viongozi wa River's United ili waombewe Caf ili wacheze mechi ya pili kwa Mkapa ili wasiingie gharama KUBWA za kwenda Nigeria Maana Hata wakienda watafungwa kwahiyo Bora sare ya hapahapa viongozi wa River's United wangewakubalia kwa Hekima.
      Sasa Pesa zinawatoka Na kufungwa kunawaumiza wote yaani WACHEZAJI, viongozi Na mashabiki pia !!!
      Tarehe 25/9/2021
      SIMBA inanafasi ya kuichapa YANGA goli ZAIDI ya MBILI .Tukutane hapa jioni siku hiyo ndipo itakuwa YANGA Kama Ngoma ya kijiji kila mtu ajipigie tu!

      Delete
    2. Tatizo siyo hela ndiyo maana tulikodi hedge nzima kupeleka na kutusubili ili kuondokana na maambukizi ya Corona. Ungekuwa wewe mikia na huyo Gabachori wenu mnaweza? Sasa hivi umeingia mkataba feki ili nipate unafuu wa nauli acheni zenu mikia nyie.

      Delete
    3. Hawana maarifa viongozi unataka wakaloge? Nop kocha Nabi nimegundua kusuka kikosi ni ngumu kwake. Beki hawajipangi vyema. Angalia goli la Dsm, mabeki walijipanga ka washambuliaji. Hakuna waliokuwa katika mstari wa goli au katika posts. Huwezi kudifend kama umejipanga kama attacker!

      Delete
  4. Kwanini Nabi hakutaja kabisa mashtaka ya kuwa hawajapata mapokezi na pia kuwa wamesingiziwa corona. Kweli huyu ni mwana michezo asiye na chuki

    ReplyDelete
  5. Huyo sifikiri kama wataendelea nae kwani hapendi fujo na ndio mana wanamrejesha Zahera kutokana na campeni zake

    ReplyDelete
  6. Nyie watu wa Simba tulien, msije mkakimbia uwanjani, kiligoncha kufa mtu kinawasubiri

    ReplyDelete
  7. Mbona hata simba manara mulikuwa mnamwamini sana Leo VP mnamponda? Yanga sio kwamba wanamkubali Bali wanatizama vituko ambavyo ninyi simba muliamini manara ndo kilakitu simba, kumbe pesa ndo kila kitu.yanga wajanja ili ninyi simba mkome kuisema yanga Bali mhamie kugombana na manara.na manara kiukweli pengo kubwa sana simba coz simba maneno ya manara yalikuwa faraja kwao pindi wakifungwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic