March 4, 2019






Kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys kimeanza michuano ya Uesfa Assist kwa kupoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Guinea.

Mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Emri Complex, ilitawaliwa na Guinea katika kipindi cha kwanza kabla ya Serengeti kuibuka katika kipindi na kuonyesha uhai katika kipindi cha pili.

Guinea ambao kwa maumbo ni wakubwa walionekana kujiamini zaidi katika kipindi cha kwanza na kupoteza nafasi nyingi za kufunga.

Wachezaji wao hasa Toure Alya na Mohamed Lamine walitawala nafasi ya kiungo na kuipa Serengeti wakati mgumu.

Hata hivyo, baada ya Lamine kutolewa katika kipindi cha pili, ilitoa nafasi kwa Serengeti kufanya vema zaidi na kutawala huku ikipoteza nafasi kadhaa za kufunga.

Serengeti Boys  itashuka dimbani tena keshokutwa Jumatano kuwavaa Australia katika mechi ya pili ya Kundi Namba Moja itakayopigwa saa 9:30 Alasiri kwa muda wa hapa unaoendana na nyumbani Tanzania.

Mechi ya mwisho ya Serengeti Boys itakuwa dhidi ya wenyeji Uturuki.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic